Get Adobe Flash player


Seven Visions were unveiled to the President, Pastor Justice Lutashobya by 2005 in 40 days fasting prayer, for to fulfill the assigments he was given. In 2006 September pastor Justice organised the launching conference to share these visions with 150 partners of the gospel. 


WMMC ilianzishwa chini  ya uongozi wa Roho Mtakatifu Mwaka 2006, Roho wa Mungu  alimwongoza Askofu Justice Lutashobya katika Maombi ya siku 40, akaanda mkutano wa kuzindua huduma hii baada ya maombi, wadhamini na wadau wengine wa walihudhuria mkutano wa kwanza wa WMMC Pale Karimjee Dar es salaam tarehe 29, Septemba 2006. Mhasisi alipata Baraka za Askofu wake ambaye ni Katibu Mkuu wa CPCT, Bishop David Mwasota.

Kwa kuwa wadhamini walitoka  madhehebu mbalimbali na tulitoka katika mapokeo mbalimbali, tulikubaliana kuacha mapokeo ya dini zetu za zamani, na katiba  za  dini zetu ili twende kueneza Injili ya Wokovu kwa kutumia Katiba Kuu ambayo ni Biblia. Tulisema tunavuka mipaka ya dini zetu na Kuvunja kuta za dini ili tuhubiri Injili kwa watu wote katika mataifa yote.

Msingi Mkuu wa  WMMC  ni INJILI NA UMISHONARI wa ndani na nje ya nchi; Hii inamaanisha kwamba WMMC  ni HUDUMA YA KITUME. Umishonari ni AGIZO tena ni AGIZO KUU lilitolewa na mwenye kulianzisha kanisa yaani Bwana Yesu Kristo kama ilivyoandikwa katika MATHAYO 28:19-20.

Hivyo kwa ujumla  WMMC inaamini katika IMANI NA NGUVU ZA KIPENTEKOSTE. Na katika Shule za huduma tumekuwa tukifundisha imani na Nguvu za kipentekoste kwa Moyo wote, kwa Nguvu zote; kwa Roho yote na  kwa akili zetu zote;  na mitaala ya mafundisho ya vyuo vyetU imeandaliwa kwa misingi ya Kipentekoste.

Mafundisho yetu ( Doctrine), lazima yajikite katika kile tunachokiamini; Lazima yatokane na msingi wa Imani ya WMMC. Kila dhehebu lililosajiliwa linayo misingi ya imani ambayo imebeba mafundisho yao NA IMANI YAO. Hatuwezi kuamini katika Mungu wa Miujiza kwa mfano, halafu mafundisho yetu yanapinga Miujiza inayotakana na Mungu wetu!!!?

Hatuwezi kuamini katika  Mungu wa Mitume na Manabii, Halafu mafundisho yetu yakapinga mitume na manabii! Hutuwezi kuamini katika Injili ya Uponyaji, halafu mafundisho yakapinga uponyaji Kwa Neno na Kwa matendo Yetu!  Biblia inasema imani lazima ijieleze kwa NENO NA KWA TENDO ( WAKOLOSAI 3:17).

LAKINI PIA HATUTATOA KIBALI ASILIMIA 100% KUFUNDISHA IMANI NA MAPOKEO YA MADHEHEBU AU HUDUMA ZINGINE, HATA KAMA NI YA KIPENTEKOSTE INAYOTOFAUTIANA NA WMMC. ISIPOKUWA IMANI YAO IWE INAFANANA NA YA WMMC AU INATOKANA NA BIBLIA.

Kwahiyo, yako mambo ya msingi katika imani ya kipentekoste ambayo tunayasimamia kama WAMISHONARI NA MITUME  WA  WORLD MIRACLE MISSION CENTRE katika siku hizi za mwisho kama ifuatavyo:

  1. Tunaamini katika Wokovu wa Yesu Kristo ambao ni zawadi kwetu kwa njia ya Neema. Tumeokolewa kwa Jina la Yesu, kwa Toba ya dhambi tulizotenda, tunaamini ya kwamba Yesu alisulubiwa  na kufa msalabani ili sisi na watu wote wanaomwamini,wakombolewe kutoka dhambini. ( Matendo 4:12; ISAYA 53)
  2. Tunaamini katika hatua tatu za wokovu: Kuhesabiwa haki baada ya kumkiri Bwana Yesu (Warumi 8:11, 1Wakoritho 6:11); Kutakaswa Baada ya Ujazo wa Roho Mtakatifu na Neno (1Wakoritho 3:16, 1Wakoritho 6:19) na Kutukuzwa wakati wa Parapanda itakapolia ( 1Thesolonike 4;17)
  3. Tunaamini katika huduma zote za Roho Mtakatifu, na Nguvu za Kipentekoste, Kulingana na kitabu chote cha Matendo ya Mitume; Hasa sura ya 1, 2, 3 na 9.
  4. Tunaamini katika Nafsi Tatu za Mungu; yaani Utatu Mtakatifu; Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. Kwamba Mungu Baba ni Mungu; Yesu Kristo ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu. (1 Yohana 5:8; Luka 3:20, Isaya 9:6; Tito 2:13)
  5. Tunaamini katika Huduma za Kitume, Kinabii, Kiinjilisti, Kichungaji na Ualimu kwamba kanisa haliwezi kushinda bila hizi huduma, kulingana na WAEFESO 4;11. Kanisa limejengwa chini ya misingi ya Kitume na Kinabii, ili kuvunja kazi za Ibilisi. ( 1Yohana3;8)
  6. Tunaamini katika mafunuo ya Roho Mtakatifu yanayothibitishwa na Biblia iliyoandikwa na yale yanayothibitishwa na Roho Mtakatifu na pia yale ambayo yatafunuliwa na kuthibitishwa na Roho wa Mungu. ( Yohana 21:25)
  7. Tunaamini katika Biblia Takatifu ( Agano la Kale na Agano Jipya); Kwamba ni Neno la Mungu liloandikwa chini ya Uongozi wa Roho Mtakatifu, Likavuviwa kwa mafundisho, maonyo, kuelekeza, kuongoza watu wote waliokoka na wasiyookoka katika Wokovu. ( 1 Petro 1:20-21).Tunaamini ya kwamba Neno halina makosa  na halishindwi ( Infallible) na limehakikishwa na Roho Mtakatifu. ( Mithali 30: 5-6)
  8. Tunaamini kwamba Mafuta, Moto, Maji, Upepo, Njiwa , Mhuri na Kunena kwa Lugha mpya ni Ishara za Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu Agano la Kale na Jipya. ( Matendo 2,  Luka 3:22, 2 Wafalme1: 9-12  na 1Samweli 16:13-14)
  9. Tunaamini katika Uponyaji wa Ki-Mungu, Tunaamini katika Mungu wa Miujiza na ishara zote za Roho Mtakatifu walizotenda manabii katika agano la kale na Jipya kwa kutumia Jina la Yesu na Nguvu za Roho Mtakatifu. (Matendo 4:13-30)
  10. Tunaamini katika ubatizo wa maji mengi kwa ajili ya toba ( Mark16:16); Ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya Utakaso ( Matendo 2:2-4); na Ubatizo wa Moto kwa ajili ya Nguvu za Kipentekoste.( Matendo 2).
  11. Tunaamini katika maombi ya kitume na kinabii kwa uongozi wa Roho Mtakatifu; kwa Jina la Yesu Kristo. Haya ni maombi ya kufunguliwa watu wenye vifungo hata baada ya kuokoka. ( YOHANA11:44).
  12. Tunaamini katika Unyakuo wa wenye haki katika siku za mwisho, Ufufuo wa Wafu, Dhiki kuu kabla ya hukumu ya mwisho; na Kwamba baada ya hukumu ya wasiohaki, Wenye haki watarithi uzima wa milele katika Nchi na Mbingu Mpya ( Ufunuo 21).
  13. Tunaamini kwamba, Bwana Yesu atarudi tena mara ya Pili, Kwamba kila jicho litamwona; Kama alivyokuja mara ya kwanza kama mwanadamu, kwa kutungwa mimba ya Roho Mtakatifu ndani ya Bikra Mariamu, akasulubiwa, akafa, akazikwa na kufufuka siku ya tatu kutoka kwa wafu, akajidhihirisha kwa wanafunzi wake siku 40; akapaa mbinguni mbele ya wanafunzi wake. ( Matendo 1:11)
  14. Tunaamini kwamba Kanisa ni mwili wa Kristo na Bibi arusi wa  Bwana Yesu, ambaye amepewa agizo la kupeleka injili kwa watu wote; katika lugha, kabila na mataifa yote na kuwafanya kuwa wanafunzi wa Yesu. ( Mathayo 28:19-20)