Get Adobe Flash player


1. Shetani Anapigwa

... ukijua mbinu hizi lazima utampiga na kupata ushindi asilimia 100. Juu ya mwamba huu Bwana Yesu amelijenga kanisa lake na mlango wa kuzimu hautalishinda. Wewe ndiye kanisa lake. PIGA VITA!

Order This Book Now



2. Mpakwa Mafuta

Mpakwa mafuta ni mtu yeyote aliyeokoka na amejazwa Roho Mtakatifu kufanya kazi ya Ufalme wa Mungu katika kiwango cha mwamini, mwanafunzi na Utume. Waaminio wanapojazwa Roho Mtakatifu, ujazwa wake unatofautiana kati ya mtu na mtu.

Order This Book Now


3. Ishara za Roho Mtakatifu

... habari za ishara ambazo Roho Mtakatifu anazitumia kutenda kazi za kifalme kwa aili ya utukufu wa Mungu. Habari hii ni ufunuo wangu niliopata kwa kufunga na kuomba.

Order This Book Now


4. Macho Saba ya Mungu

Ndani ya upako kuna siri kubwa sana, kuna nguvu, hekima, ufahamu, uweza, maarifa na ufunuo wa hali ya juu sana wa ki-Mungu. Kwa mujibu wa Biblia, ndani ya mpakwa mafuta kuna Roho Saba za Mungu ili kazi ya huduma itendeke.

Order This Book Now


5. Tetemeko La Kiroho Linakuja Tanzania

Mchungaji Lutashobya ambaye ni mwandishi anaamini katika UNABII MKUBWA unaokwenda kutimia kabla ya kurudi kwa Bwana Yesu ni TETEMEKO LA WOKOVU NA HUKUMU linalokuja kwa ajili ya nchi yetu Tanzania.

Order This Book Now


6. Ukombozi wa Mateka wa Tanzania

Mchungaji Lutashobya (mwandishi) anakushirikisha katika hali ya vita ya kiroho inayoendelea katika Taifa letu la Tanzania na matokeo yake juu ya watanzania. Watanzania na wakristo wengi wako UTUMWANI kiroho na kiuchumi wanawatumikia akina FARAO na HERODE ambao wamewafanya mateka kwa kutumia mapepo ya aina mbalimbali pamoja na miungu ya kigeni.

Order This Book Now


7. Maombi ya Tetemeko

Tetemeko la maombi linakuja Tanzania kufanya mapinduzi ya kiroho ndani ya nchi ya Tanzania ili kuliandaa Taifa na kanisa kwa aili ya KURUDI KWA YESU MARA YA PILI.

Order This Book Now


8. Ndoa ni Ufalme Kamili.


... Mchungaji Lutashobya anaamini kuwa Mungu alisimika ufalme katika ndoa alipofanya tamko, kusema zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha, MKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Kwa tamko hili juu ndoa alikuwa anatoa MAMLAKA JUU UFALME WAKE DUNIANI, ili utawale sawasawa na mapenzi yake.

Order This Book Now



9. Maombi ya Kufunga.


... Katika kitabu hiki, Mchungaji Lutashobya anatoa hakikisho na matokeo yake kuhusu njia za kufunga, na jinsi ya kufungua; kwa sababu palipo na kufunga kuna kufungua pia. Katika maombi ya kufunga kuna mambo tunayofungulia na kuna mambo tunayafunga; kuna milango tunafunga na kuna milango tunaifungua; kuna roho tunafunga na kuna roho tunafungulia; kuna kazi tunafungua na kuna kazi tunafunga.

Order This Book Now



10. Moyo wa Injili.


... . Mwandishi wa Moyo wa Injili ni mhubiri wa INJILI kwa zaidi ya miaka 14 sasa. Amekuwa akifundisha ujumbe huu kwa machozi katika shule za huduma, shule za maombi na semina za wachungaji katika vijiji na miji. Alipofundisha ujumbe huu katika shule ya Huduma kwa watumishi wa Kagera mwezi wa Aprili 2013, kuwa na Moyo Mkuu kwa ajili ya Injili; Wachungaji waliomboleza muda wote wa semina. Wingu lililobeba mvua ya Roho Mtakatifu; mafuta ya Roho Mtakatifu liliwafunika wachungaji. Moyo wa Injili na umisheni umejaa roho ya kueneza, kutetea na kuilinda imani ya Injili. Shabaha ya moyo wa Injili ni KUOKOA ROHO ZILIZOPOTEA.

Order This Book Now



11. Maombi ya Mapinduzi.


... Mzigo wa maombi ya mapinduzi umejengeka kwa Mchungaji Justice Lutashobya toka mwezi Juni, 2011 alipofanya mapinduzi katika maombi yake. Badala ya kuomba kwa ajili huduma yake na familia, sasa alifunga muda wa miezi saba na kuanza kufanya maombi ya usiku kwa ajili ya Taifa. Safari hii alikuwa anafunga na kuomba usiku kuanzia saa tano usiku kila hadi saa nane au tisa wakati mwingine. Maombi ya mapinduzi juu ya TAIFA, KABILA NA LUGHA yalitawala na yanaendelea kutawala moyo wake, hadi akawaka katika moto wa maombi. Ndipo akapewa ujumbe katika kitabu hiki.

Order This Book Now



12. Huduma za Roho Mtakatifu.


... Wakristo wengi wanajua kazi za Roho Mtakatifu kwa sehemu ndogo ya KIROHO. Wanafikiri Roho Mtakatifu anafanya Kazi za Kiroho tu, hivyo nje ya hapo Roho Mtakatifu hafanyi zaidi. Naomba utambue kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu anayetawala DUNIANI, MBINGUNI NA KUZIMU maana ndiye aliyeviumba. Mbiguni yupo anafanya huduma, Duniani yupo anafanya Huduma. Anayo mamlaka na KUZIMU kwa sababu ndiye aliyemfufua YESU KUTOKA KWA WAFU. ROHO WA UFUFUO NI ROHO MTAKATIFU.

Order This Book Now