Get Adobe Flash player

Church planting is one the seven visions of World Miracle Mission Center. We have worked with many faith organisations and churches from 2006 to facilitate church planting mission in Tanzania urban and rural areas. Church planting missions includes organising for evangelistic crusades and conferences, conducting schools of ministry for pastors, church designs and construction drawings, cost planning and supervision services.


DAR ES SALAAM MISSION

In Dar es salaam we have organised and Supported many churches since 2007. We designed more than 10 churches of Tanzania Assemblies of God as part of church planting support in 2008 including cost advice and planning. We organised , designed and financed the roof structure for FPCT church Kiluvya about 50 % of the total cost.


CONTINOUS CHURCH - BOKO, DAR ES SALAAM

Kanisa la  Continous  lilipandwa Mwaka 2015, na  Mchungaji na Mama Mchungaji Peter na Neema Wesire  ambao  ndiyo Wachungaji wa Kanisa lililoko mtaa wa Maliasili Boko. Kanisa hili lilianzishwa na watumishi hawa ambao wanayo huduma ya utume na uinjilisti baada ya kufanya ibada ya kwanza Mwaka 2015.

Kanisa la Continous limekua  na kufikia washirika zaidi ya 200 ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake. Na mchungaji Peter na Neema wamefuata maelekezo ya uongozi wa WMMC na Roho Mtakatifu. Kanisa asilimia zaidi ya 70 wamejaa Roho Mtakatifu.  Continous Ministry ndiyo maono ya kanisa hili ambalo linakuwa kasi, siri yake kubwa ni Huduma za maombezi, Kujali watu wote bila ubaguzi wa rangi, kabila au dini na Upendo wa Agape. Ukiwa na Tatizo watakufikia hapo ulipo kukuletea msaada. Unakaribishwa katika Upendo wa Kristo kwenye ibada za Continous; Mungu atakutembelea.

WMMC inaamini huduma ya Kristo lazima itatue matatizo ya watu katika jamii; kwa sababu Kristo alikuja kutatua matatizo ya DHAMBI; MAGONJWA NA KIFO.


USSOKE CHURCH - TABORA

Kanisa la URAMBO ni kanisa mama lililopandwa na  WMMC kwa ushirikiano na Mchungaji  Obed Karoli Mwaka 2013, baada ya mkutano wa injili Kuhubiriwa katika kijiji Cha Usongelani. Mwaka 2013 Mchungaji Obed  Karoli aliomba uongozi wa WMMC kuandaa na kuhubiri mkutano wa nje, kwa malengo ya kupanda Kanisa.

Mchungaji Lutashobya alimpa maelekezo kwamba ya kujenga hema la mkutano wa nje na Hema hilo halikutoka ndilo liliendelea kuwa jengo la kanisa. Na haya ndiyo mafunuo ya  WMMC katika mpango wa kupanda makanisa kulingana na mwongozo namba 1 wa kaupanda makanisa.

Baada ya kupata uwanja mwingine Uyui, Mchungaji Obed alipanda Tawi la Uyui, lililoko katika kijiji cha Usungu Utemini, Kata ya Ndono,Tarafa ya Ilolangulu, Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora.

Kanisa la Urambo limekuwa  na kufikia washirika zaidi ya 100. Na mchungaji Obed amefuata maelekezo ya uongozi wa WMMC na Roho Mtakatifu. Kanisa asilimia zaidi ya 50 wamejaa Roho Mtakatifu.  Mwaka 2016 Mchungaji Lutashobya  na mitume wa WMMC waliandaa mkutano wa nje na semina


JERUSALEM CHURCH - MULEBA

Kanisa la Jerusalemu lilipandwa Mwaka 2013, na mtume Johanesia Rwetatila ambaye anayo huduma ya utume baada ya kufanya ibada ya kwanza tarehe Novemba 13, 2013, katika mtaa wa Kahauza, ofisi za Red Cross Muleba.

World Miracle Mission Centre ilifanya mkutano wa nje mwaka 2014, na watu zaidi 100 waliokoka  na kuingia katika ufalme wa Mungu. Tangu 2014, kanisa limeongezeka kutoka watu 50 na kufikia zaidi ya 100 ndani ya mwaka mmoja. Mchungaji Lutashobya alifanya mikutano ya ndani Machi- hadi May mwaka 2015 na kufanikiwa kujenga jeshi la watendakazi na wamishonari. Kanisa hili linajulikana kama kanisa la Maombezi, na watu wengi wamefunguliwa.


UKOMBOZI CHURCH - MULEBA

Kanisa la Ukombozi lilipandwa Mwaka 2015, na Mtume Brighton Ibrahimu George  ambaye  ndiye Mchungaji wa Kanisa, Tawi la Saa ya Ukombozi, lililoko mtaa wa Buhimba. Kanisa hili lilianzishwa na mtumishi huyu ambaye anayo huduma ya utume baada ya kufanya ibada ya kwanza tarehe May 5, 2015, katika mtaa wa Buhimba, Muleba Mjini.

World Miracle Mission Centre ilifanya mkutano wa ndani 2015, katika operesheni ya Mbio za kinabii. Kanisa lina washirika zaidi 50 sasa na limefungua matawi pale Nshamba na Karagwe.

Mwaka 2015 WMMC chini ya uongozi wa Mchungaji Lutashobya kanisa lilifanya mikutano ya ndani Machi- hadi May mwaka 2015 na kufanikiwa kujenga jeshi la watendakazi na wamishonari. Linajulikana kama kanisa la Ukombozi, na watu wengi wamefunguliwa katika Halmashauri ya Muleba.


KANISA LA CHUO EFO - LYAMBA MGONGO, BUKOMBE GEITA

Kanisa la Chuo cha Elumaka Foundation lilipandwa Mwaka 2015, na Mitume wa WMMC; linachungwa na Mchungaji Hilda kwa ushirikiano na Mchungaji Flora.  Hawa ndiyo Wachungaji wa Kanisa, Tawi la EFO Dispensary and Nursing college, lililoko katika kijiji cha Lyamba Mgongo. Mchungaji Obed Karoli ndiye mchungaji kiongozi wa kanisa hili tangu Mwaka 2016.

Kanisa hili lilianzishwa na mitume wa WMMC ambao wanayo huduma ya utume baada ya kufanya ibada ya kwanza tarehe Novemba 13, 2015, katika kata ya Lyamba Mgongo, kwenye kituo cha afya cha Elumaka Foundation-Bukombe.

World Miracle Mission Centre ilifanya mkutano wa ndani 2015, katika operesheni ya Mbio za kinabii. Askofu Mkuu, Justice Lutashobya alibatiza wahongofu wapya katika mbio za kinabii ambazo zinafanyika mara 3 kila mwaka. Kanisa lina washirika zaidi 50 sasa  WMMC  inakusudia kulitoa kanisa  ili watu wote wawe za kushiriki ibada zote.

Mwaka 2015 WMMC chini ya uongozi wa Mchungaji Lutashobya kanisa lilifanya mikutano ya ndani Machi- hadi May mwaka 2015 na kufanikiwa kujenga jeshi la watendakazi na wamishonari. Linajulikana kama  CHAPEL YA WANAFUNZI, na watu wengi wamefunguliwa.


KANISA LA AGOSMI - GUNGU, KIGOMA

Kanisa la AGOSMI, Kigoma lilipandwa Mwaka 2015, na Mchungaji ALEX NESTORY OBED; ambaye  ndiye Mchungaji kiongozi wa Kituo Chetu cha  Umishonari, Injili na Huduma za jamii cha African Good Samaritan Ministries Foundation. Na Ndugu ALEX ISSA RUHANA ni Katibu Mkuu wa Kituo chetu cha AGOSMI kilichopo katika Wilaya yako ya Kigoma, Mkoa  wa Kigoma. Kituo kipo Mtaa wa Masanga, Kata ya Gungu.

World Miracle Mission Centre ilifanya mkutano wa ndani  mwezi Octoba, 2014, katika  Shule za Huduma. Kanisa lina washirika zaidi 20  na linaongezeka kwa kasi.

Risala ya AGOSMI 2014 ...